.WATOTO zaidi ya 478,010 wenye umri chini ya miaka nane wanategemewa kupata chanjo ya polio awamu ya pili mkoani Songwe inayotegemewa kufanyika kuanzia novemba 2, hadi 5 mwaka huu 2023.
Akifungua kikao cha taarifa ya ya kampeni ya chanjo ya polio awamu ya pili inayotarajia kuendeshwa mikoa sita Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Francis Michael amesema lengo la kufanya kampeni ni kutokana na ugonjwa wa polio ambavyo umekuwa tishio kwa miaka mingi katika nchi nyingi Duniani.
"Ugonjwa wa polio hauna tiba lakini unaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya matone au sindano, hivyo njia kuu ya kujikinga na ugonjwa wa polio ni kupitia chanjo ya polio ambayo imekuwa ikitolewa muda mrefu kwa watoto chini ya miaka mitano" amesema .
Alisema kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata mgonjwa wa polio mwezi julai mwaka 1996, lakini hivi karibuni nchi jirani na Tanzania zimekumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa polio ikiwemo Malawi, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
"Tanzania tumepata kisa kimoja cha mtoto wa umri wa mwaka mmoja aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo katika mkoa wa Rukwa" alisema Dkt Francis.
Mganga mkuu wa mkoa wa Songwe Dokta Boniface Kasululu amesema utekelezaji wa kampeni ya polio awamu ya kwanza iliyofanyika September 21, hadi 24 mwaka huu 2023 walengwa wenye umri chini ya miaka nane (8) walikuwa 402,644 .
Amesema lakini kwa awamu hiyo ya kwanza jumla ya watoto 478,010 walifikiwa sawa na asilimia 118.7.
"Walengwa ni watoto wote wenye umri chini ya ya miaka 8, waliozaliwa kuanzia mwaka 2016, ambapo kwa mkoa wa Songwe ni watoto wote waliopata chanjo awamu ya kwanza wasiopungua 478010" amesema Dokta Kasululu.
Mwakilishi kutoka Tamisemi Carle Lyimo amesema mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikoa ambayo imefanya vizuri katika chanjo ya awamu ya kwanza kwa kufikia 118.7.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.