WATUMISHI TUJIANDAE KUSTAFU, RAS SENEDA.
SONGWE: Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda amewataka watumishi wenzake kujiandaa kustafu katika utumishi wa umma ili muda utakapofika wa kustafu wasipate shida.
Bi. Happiness Seneda amesema mtumishi unapopata barua ya ajira ya kwanza ndio muda wa kuanza kujiandaa kustafu, hivyo amewataka maafisa utumishi kuwapa elimu watumishi wote kujiandaa kustafu.
"Haipendezi mtumishi unafika umri wa miaka zaidi ya 50 ndio unaanza kujifunza kufuga kuku, kulima au biashara wakati hivi unapaswa kujifunza ukiwa kazini" Bi. Happiness Seneda.
Katibu Tawala Mkoa, Bi. Happiness Seneda amesema mtumishi anastafu anapata kiinuo mgongo badala ya kimuinue kweli matokeo yake kina mvunja mgongo kwa kuanza kazi ambazo hajawai kufanya.
Sifa kubwa ya ujasilimali ni kufanya mara kwa mara ili iweze kufanikiwa ili siku ukistafu zile fedha zinakusaidia kwenye kwenye mtaji wa kazi yako, sasa hujafanya ujasiliamali ukiwa na umri wa miaka 15, 30 au 50 ndio uje ufanye umestafu hii haiwezekani, amesema Bi. Happiness Seneda.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.