Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Bi. Nuru Waziri Kindamba kuanza mchakato wa kuifanya Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kuwa na hadhi ya kidato cha Tano na Sita (Advance).
Waziri Mkuu ameyasema hayo Novemba 23, 2023 wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo alipata fursa ya kukagua ujenzi wa majengo ya shule hiyo huku alionesha kuridhishwa na kiwango cha ubora wa mradi huo ambao umegharimu zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 500 za kitanzania.
Akihutubia wananchi mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa pesa nyingi sana kutekeleza miradi ya maendeleo hususan katika nyanja ya Elimu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itahakikisha majengo mapya ya Maabara katika shule ya wasichana ya Ileje (Ileje Girls) inapata vifaa vya kisasa ili iweze kuwa na tija kwa wanafunzi na kusaidia katima utoaji wa elimu bora yenye matokeo chanya kwa wanafunzi.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.