Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB), Ameelezea furaha yake juu ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Msingi Dr Samia SH iliyopo katika Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe. Ujenzi huo umetekelezwa chini ya Mradi wa BOOST, ambao una lengo la kuboresha ya Shule za Msingi nchini.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Songwe, Waziri Mkuu ameipongeza Shule ya Dr Samia SH kwa kuwa mfano bora wa shule inayotia moyo na kuvutia. Amesifia juhudi za viongozi wa ngazi ya mkoa na ngazi ya wilaya kwa kusimamia mradi huo hadi kuifanya shule hiyo kuwa bora na yenye hadhi ya kitaifa.
Aidha, Ameelezea kuvutiwa kwake na muundo mzuri wa shule hiyo, akibainisha kuwa inapaswa kuwa kigezo kwa shule nyingine. Ameonekana kuvutiwa na mandhari mazuri, kuanzia ofisi za walimu hadi madarasa, ambayo amesema ni mazingira yanayowavutia wanafunzi kuhudhuria shuleni na hivyo kuwapa motisha na uwezo mkubwa wa kusoma na kujifunza.
Waziri Mkuu pia ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Shule na Afisa Elimu kwa utendaji wao mzuri na uongozi wao katika kusimamia shule hiyo. Amesema mchango wao umesaidia kufanikisha malengo ya mradi na kufanya Shule ya Dr Samia SH kuwa taasisi inayojivunia na inayoheshimika kitaifa
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.