WHO KUONGEZA NGUVU UCHANJAJI WA CHANJO YA UVIKO 19 SONGWE
SONGWE: Shirika la Afya Duniani (WHO) kuongeza nguvu YA Uchanjaji wa chanjo ya UVIKO-19 Mkoa wa Songwe.
Hayo yamesemwa na muwakilishi wa WHO, Dkt. Onekwe Chima alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ofisini kwake, Julai 14.
Dkt. Onekwe Chima amesema wananchi wanahitaji elimu ya kutosha kuhusu chanjo ya uviko 19, ushirikiano wa kutosha kwa ngazi zote kutoka vijiji hadi Mkoa na njia mbadala ya kuwafikia walengwa hasa pale wanapokuwa mbali na vituo vya afya kwa ajili ya kupata chanjo ya UVIKO-19.
"Tumetoka Mkoa wa Manyara tumeona jinsi wananchi walivyoitikia chanjo na Manyara ilikuwa ya mwisho lakini saizi imetoka uko na saizi imebaki Songwe ndio Mkoa wa mwisho" Dkt. Onekwe Chima.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rose Alfred amesema awamu hii ya sasa wamejipanga kuhakikisha kila kituo cha Afya kinatoa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 na kuripoti kwa mamlaka husika kila siku, ikiwa ni pamoja na kufanya huduma mkoba ili kuweza kuwafikia wananchi waliombali na vituo vya kutolea huduma za afya, kupita Nyumba kwa nyumba na sehemu zote ambazo kunamkusanyiko wa watu ili kuhakikisha kila mlengwa anapatiwa chanjo ya UVIKO-19.
"Kwa wale ambao tutawapatia chanjo ya UVIKO-19 inayohitaji dosi mbili kukakilisha dosi, tutaweka utaratibu wa kuwafatilia na kuwakumbusha pale dozi ya pili inapohitajika ili kuweza kukamilisha dosi na kuwakinga wananchi wengi dhidi ya maambumizo ya UVIKO-19" Dkt. Rose
Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO-19 na watahakikisha chanjo inapatikana kote ndani ya Songwe.
Pia, Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa viongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa kutoa elimu kwa wananchi na kuhamasisha kampeni ya chanjo ya UVIKO-19.
Kwa sasa Mkoa wa Songwe unashika nafasi ya Mwisho katika utoaji chanjo ya UVIKO-19 kitaifa.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.