YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA TATHMINI YA MAHITAJI YA VYUMBA VYA MADARASA NA MADAWATI MKOA WA SONGWE
Posted on: November 22nd, 2018
Kikao hiki cha tathmini ni maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2019, - Afisa Elimu Mkoa Juma Mhina.
Wanafunzi 22,057 ikiwa wavulana 10,300 na wasichana 11,757 walifanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi mkoa wa Songwe Septemba 5-6, 2018, - Afisa Elimu Mkoa Juma Mhina.
Matokeo yaliyotoka 23 Oktoba, 2018 yameonyesha ufaulu kwa ngazi ya Mkoa umepanda kwa asilimia 10 huku wanafunzi 16,291 wakifaulu kujiunga na kidato cha kwanza ikiwa wavulana ni 7,436 na wasichana 8,855, - Afisa Elimu Mkoa Juma Mhina.
Mkoa unahitaji madarasa 373 kwa ajili ya wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza 2019, yaliyopo ni 219 hivyo upungufu ni madarasa 154, aidha mahitaji ya madawati ni 14,846 yaliyopo ni 6,076 na hivyo upungufu ni madawati 8,770, - Afisa Elimu Mkoa Juma Mhina.
Kwa namna yoyote ile Januari 2019 wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lazima waanze shule,- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila.
Mkoa utafanya ufuatiliaji wa maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2019 hususani suala la vyumba vya madarasa na madawati, - Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila.
Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zifanye operesheni ya kuhakikisha vyumba vya madarasi na madawati yanakamilika ndani ya mwezi mmoja, - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus E. Mwangela.
Halmashauri zote ziwasilishe ndani ya siku tano mpango wa utekelezaji maandalizi ya mapokezi ya Kidato cha kwanza 2019 hususani namna ya kukamilisha vyumba vya madarasa na madawati,- Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus E. Mwangela.