Soko la madini Mkoani Songwe litakuwa Wilayani Songwe na tunaamini ya kwamba wale waliozoea biashara za ujanja ujanja watakasirika, watabeza na kuhujumu lakini Kamati ya Usalama Wilaya ya Songwe imejipanga kuhakikisha hili litakamilika- DC Songwe Samuel Jeremia
Baada ya tarehe 8 Mei, 2019 yeyote atayeuza madini mkoani Songwe nje ya Soko la madini la Mkoa anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni kutaifishwa mali, kufunga mwaka mmoja au vyote viwili kwahiyo nina watahadharisha tufuate sheria Pia Kamati ya Usalama Wilaya tutaanza kufanya ukaguzi na yeyote atayekamatwa atachukuliwa hatua za kisheria- DC Songwe Samuel Jeremia
Kila siku kutakuwa na Kilogramu tatu za dhahabu ambazo zitaleta mauzo ya shilingi milioni 270 na kwa mwezi itakuwa bilioni 6.7, fedha ya serikali itakuwa milioni 472 na halmashauri ni milioni 20.2 kwa mwezi ambapo fedha hizi zilikuwa hazipatikani kabisa- DC Songwe Samuel Jeremia.
Soko hili la madini litawasadia hasa wachimbachi wadogo kutambulika na kuzuia utoroshaji wa madini tuna Imani tatizo la kudhulumiana na kupunjana litakwisha hivyo nawasihi wote wanaohusika na sekta ya madini kulitumia- RC Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
Nawapongeza uongozi na wanachama wote wa chama cha wachimbaji wadogo kwa kuonyesha nia na kukubali kulipokea soko hili madini, mmeonyesha uzalendo na sisi tutashirikiana nanyi, kwani tunatambua kuwa soko hili ni kiunganishi kati ya wauzaji na wachimbaji RC Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
Mkoa wa Songwe una leseni 24 za utafiti wa madini, 101 uchimbaji mdogo, 5 za wachimbaji wa kati na kwa mwezi Machi Wilaya ya Songwe ilizalisha kilogramu za dhahabu 411.1- RC Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
Umuhimu wa soko la madini utakuwa ni uwepo wa soko la uhakika la madini ambalo litakuwa na malipo halali, soko litaondoa tatizo la kudhulumiwa na kupunjwa, Uwezekano wa kuibiwa hautakuwepo, Bei itaratibiwa na serikali na hiyvo kumnufaisha muuzaji na mnunuzi na litawezesha uwepo wa takwimu za uhakika- RC Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
Nawaelekeza Tume ya Madini na Wakala wa Vipimo kuhakikisha wanasimamia vifaa na taratibu zitakazotumika katika kupima madini hayo ili kuepuka malalamiko RC Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela.
Katibu wa Chama cha wachimbaji wadogo (SOREFA) Mkoani Songwe Elias Pangani amesema wachimbaji wadogo wako radhi na ni walipaji wazuri wa Kodi ya Serikali, wanaipongeza serikali kwa kuanzisha soko la madini kwani wamekuwa wakihangaika kutafuta masoko ya uhakika.
Kuzalisha kitu bila ya uwepo wa masoko ya uhakika ni kazi ngumu, kwahiyo wazo la uanzishwaji wa masoko ya madini ni jambo la kuungwa mkono, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ambaye ndiye muasisi wa wazo hili, nasisi kama Mamlaka ya Mapato Nchini tunaahidi na tuko tayari kutoa ushirikiano- Naibu Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) Msafiri Mbibo
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.