ZAHANATI YA NJELENJE KUANZA KUTOA HUDUMA JUNI 2023.
SONGWE: Wananchi wa kitongoji cha Njelenje kilichopo kijiji cha Mbangala Kata ya Mbangala Halmashauri ya Wilaya ya Songwe pamoja na maeneo jirani ya kibaoni, mteka, kwa yanga, nzega na kasisi kuanza kunufaika na huduma za Afya ifikapo Juni 2023 baada ya Zahanati yao kukamilika kwa 100%.
Akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Songwe, Ephrem Mgimba amesema Serikali ya awamu sita imetoa fedha Milioni 50 za ukamilishaji wa Boma la Zahanati ya Njelenje baada ya wananchi wa Njelenje kwa nguvu zao walifanikiwa kujenga Boma la thamani ya milioni 14.
Ephrem Mgimba ametaja huduma ambazo zitaanza kutolewa ni kliniki kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano, kujifungua kwa njia ya kawaida na huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje.
Kuzenza Magolanga mwananchi wa kitongoji cha Njelenje amesema anafuraha kuona Serikali inawasogezea huduma ya Afya kwani hadi sasa wanatumia shilingi 40,000 za usafiri wa pikipiki kufuata huduma za Afya makao makuu ya Kijiji chao cha Mbangala na Wilayani Mkwajuni.
Benson Lyanga mkazi wa kitongoji cha Njelenje ametoa wito kwa Serikali kuharakiaha kuwapeleka watalamu wa Afya katika Zahanati ya Njelenje ili waweze kuokoa maisha ya wananchi wa Njelenje.
Akitoa majibu ya Serikali, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Ndg. Vanscar Kulanga amesema huduma za matibabu zitaanza ifikapo Juni 2023 ili kufanikisha lengo la Serikali kwa wananchi wa Njelenje.
"Hapa tunataka ifikapo Juni 2023 muanze kutibiwa, muwakute watalamu, mzikute Dawa, mama wajawazito waanze kujifungulia hapa kwa usalama" Ndg. Vanscar Kulanga Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Aidha, Ndg. Vanscar Kulanga amewapongeza wananchi wa Njelenje kwa moyo wao wa kujitolea nguvu kazi za thamani ya milioni 14 walizotumia kuinua Boma la Zahanati na kumuomba Mwenyekiti wa kijiji kuendelea na moyo huo kwenye miradi mbalimbali ambayo italetwa na Serikali.
MWISHO.
2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi
Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE
Simu: 025 2580305
Simu ya Kiganjani: 025 2580305
Barua pepe: ras@songwe.go.tz
Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.