• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
SONGWE REGION
SONGWE REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa MKOA WA SONGWE

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Sehemu
      • Mipango na Uratibu
      • Idara ya Elimu
      • Huduma za Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
  • Wilaya
    • Mbozi DC
    • Songwe DC
    • Momba DC
    • Ileje DC
  • Halmashauri
    • Mbozi
    • Ileje
    • Momba
    • Songwe
    • Tunduma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Mifugo
    • Madini
    • Kilimo
    • Biashara
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya na Ustawi Wa Jamii
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma ya Mifugo na Uvuvi
    • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
    • Mipango na Takwimu
    • Ujenzi
  • Machapisho
    • Sheria
    • Miongozo
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Utaratibu
    • Mpango Mkakati
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Wanyiha


    

Chifu (Mwene) Nzunda kiongozi mkuu wa Wanyiha


HISTORIA. 

Wanyiha ni kabila ambalo linapatikana katika wilaya ya Mbozi na linachukua robo tatu (75%) ya wakazi wa wilaya ya Mbozi. Mbali na Wanyiha, Mbozi ina makabila mengine ambayo huchukua robo (25%) ya wakazi wote.  Makabila hayo ni Wandali kutoka wilaya jirani ya Ileje, Wamalila na Wasafwa kutoka wilaya ya Mbeya, Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wabungu kutoka Wilaya ya Chunya na Wasangu kutoka Mbarali.  Makabila mengine yanayopatikana Mbozi ni Wakinga, Wahehe, Wabena, Wafipa, Wangoni na mengineyo mengi.

Historia inaonyesha hapo zamani Wanyiha walikuwa na machifu wakubwa watatu tu ambao walikuwa na wasaidizi wao.  Machifu hao walikuwa ni Mwene Nzunda, Mwene Mwamlima na Mwene Nzowa.  Kwa kuwa maeneo ya kiutawala yalikuwa makubwa, wasaidizi wa machifu walitumika kama watawala wadogo.  Wasaidizi hao walijulikana kwa Kinyiha ‘Abhahombe’.  Kazi hii haikuwa na mshahara wowote japo kulikuwa na eneo kubwa la kutawala wakaamua kuwatawaza wasaidizi wao kuwa machifu ili kurahisisha kazi za kiutawala.  Hadi sasa zaidi ya koo 20 ambazo awali zilikuwa zinasaidia shughuli za kichifu za kinyiha sasa ni koo za kichifu. 

UTATUZI WA MIGOGORO

Kwa Wanyiha walikuwa na mbinu mbalimbali za kutatua migogoro yao.  Mbinu kubwa iliyokuwa ikitumiwa na wazee kutatua migogoro ilikuwa ni vikao ambavyo viliitishwa mara tu wanapoona kuna jambo liko kinyume na mila au maadili katika jamii.  Vikao hivyo viliweza hata kutoa adhabu kwa mtu aliyebainika kuwa mkorofi na kufanya wengine waogope kufanya mambo yanayokatazwa na wazee.  Baadhi ya adhabu zilizotolewa ni kuchapwa viboko hadharani, kununua pombe, kulipa fedha na kulipa mbuzi.

Vikao hivyo vilitegemea sana mkosaji anavyokubali au kukataa kosa Mfano walikuwa wanatuma mtu kumwita Yule aliyekosa kuhudhuria kikao , kabla ya kwenda alikuwa naye anamrudishia majibu Yule aliye mletea ujumbe kuhusu kumuomba radhi kwa wazee wa mila.Hali hiyo ilikuwa inapunguza hasira kwa wazee hivyo hata adhabu haikuwa kali kama yule aliyeleta jeuri.

Njia hii ndio iliyowawezesha kutatua migogoro yote ikiwa ni ile ya ndoa, mtu kushikwa ugoni, Ardhi, uharifu wa Mazingira.Pia ikumbukwe na kuwqa kosa linapofanywa na mtu lilichukuliwa kama kosa la ukoo mzima hivyo lilifanya ukoo kuonyana wao kwa wao hata kabla kuitwa na wazee wa mila.

Kulingana na mwingiliano wa sasa na watu kudharau mila, nguvu ya wazee wa mila ya kutatua migogoro yao wenyewe na kutoa adhabu imepotea na kuwafanya pale wanapopata tatizo na kushughulikia bila kufikia muafaka kuirushia serikali ili kumaliza kwa njia ya mahakama au vyombo vingine vya kisheria.

 

HIFADHI YA MAZINGIRA

Wanyiha huamini kuwa maeneo ambayo yana chemichemi huwa yana nyoka mkubwa ambaye ndiye anayesaidia upatikanaji wa maji hayo na kuwa ukimuua nyoka huyo eneo hilo halitakuwa na maji tena.  Kutokana na imani hiyo eneo hilo lilichukuliwa katika uangalizi mkubwa na hakuna mtu aliyeruhusiwa kukata miti au kuua nyoka yoyote aliyeonekana eneo hilo na kufanya vyanzo vya maji kulindwa  na hivyo kuwa katika hali ya usalama ukilinganisha na hali ya sasa.

Si hivyo tu, kabila hili linaamini sana mizimu na watu wenye mizimu hujengewa imani sana kuwa ni watu wenye uono na hutoa msaada kwa jamii pale mtu anapoonewa hususani kwa njia ya ushirikina kwa kutoa dawa ambazo hutokana na miti.  Shughuli za watu wenye mizimu hufanyika porini kutokana na kuwa na imani hiyo wanaamini kuharibu misitu kutafanya watu wenye mizimu kushindwa kutatua matatizo yao kwani dawa hazitapatikana.

Ukataji wa miti aina ya mibula haukuruhusiwa kabisa kwani miti hiyo iliaminika kuwa na utabiri wa kujua kama ni mwaka wa njaa au la. Mibula ikizaa sana matunda wazee walichukulia kuwa mwaka huo ni mwaka wa njaa na matunda hayo yalikuwa yakitumika kama chakula wakati wa njaa pia walitumia juisi iliyotokana na mibula kwa ajili ya kuweka kwenye uji kama sukari.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI.

Wanyiha walijishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na uhunzi.  Katika kilimo walilima mazao kama ulezi ambalo lilikuwa zao la chakula, walilima maharage na baadaye baada ya kuletwa mazao mengine kama mahindi, karanga, kahawa waliendelea kulima.  Pia walikuwa wanafuga wanyama kama vile mbuzi, ng’ombe, punda, kuku.

Baadhi ya wengine walijishughulisha na kazi ya uhunzi ambao ndio waliokuwa wanatengeneza zana mbalimbali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya shughuli za kilimo. Zana zilizotengenezwa zilikuwa ni mishale, mikuki, shoka, visu na majembe.  Ufundi huu umeendelea hadi leo wapo watu katika kabila hili la Wanyiha wanaoshughulika na uhunzi kama kazi inayowapatia kipato



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI January 30, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA SAINI MRADI WA ZAIDI YA BILIONI 119.9 UJENZI WA MRADI WA MAJI TUNDUMA VWAWA

    March 20, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA ILEJE MHE. FARIDA MGOMI KWA NIABA YA MKUU WA MKOA AFUNGUA HUDUMA YA WIKI YA SHERIA MKOANI SONGWE

    January 25, 2025
  • TASAF MKOA WA SONGWE IMEFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI NA KUJIONEA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANUFAIKA WA TASAF MOMBA

    January 03, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI SONGWE.

    November 07, 2024
  • Angalia zote

Video

ELIMU KWA WATOTO KIPINDI CHA CORONA
Video za Ziada

Kurasa za Karibu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • SALARY SLIP PORTAL
  • AJIRA

Kurasa Mashuhuri

  • IKULU
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    2 Nselewa Mkoani RD, 54180 Mlowo-Mbozi

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 23 SONGWE

    Simu: 025 2580305

    Simu ya Kiganjani: 025 2580305

    Barua pepe: ras@songwe.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

writingMasterThesis

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki©2020 Mkoa wa Songwe.Haki Zote Zimehifadhiwa.